Namna ya kutengeneza blog ya kukuingizia kipato (pesa) mtandaoni


Blogging
ni kitendo cha kutengeneza machapisho,taarifa,kurasa na matukio kwa kutumia intaneri kama media.

Mtu anayetengeneza blog ama kufanya blogging anaitwa blogger.
Mfano wa bloggers ni dj mwanga(djmwanga.com) beka boy (bekaboy.com) Ramso_pro (bongoempire.com , byforums.com , wavudigital.com) issa michuzi (michuziblog.com)

Blog inaundwa na nini?

1.domain
Hii ni prefix inayowakilisha blog mfano .com , .net , .org
Hii ni kusema kuwa domain ni jina(link kuu) la tovuti yako mfano djmwanga.com , bongoempire.com , tanzaniatech.com hizo ni domain.

2.Blog editor / blogging platform
Hii ni platform/tovuti unayotumia kutengeneza , kuedit ,kumanage na kucontrol blog yako ambapo sehemu hizi ni kama vile wordpress.com , blogger.com huku ndiko unaunda blog yako kisha unaiunganisha na domain yako ili ifanye kazi.
Kiufupi blog editor ndiko utakopost habari,nyimbo,taarifa na kurasa pia kusimamia tovuti yako kwa ujumla.
Wordpress ndiyo platform nzuri zaidi kulinganisha na zingine.

3.blog theme / template
Huu ni muonekano wa blog yako ikimaanisha huu ndio unawakilisha namna blog yako itakavyooneka pia vipengele vitajipangaje katika blog yako.

4.Hosting
Hapa ni sehemu ambapo mafaili ya blog yako yataifadhiwa pia blog editor yako / platform ambayo ni wordpress ndiko itakoshikiliwa na kuunganishwa na domain yako.
Hii inahipa blog uharaka wa kufunguka na huduma za ziada.
*Blog inaingizaje pesa ?*

Blog kama zilivyo media zingine njia kuu ya kuingiza pesa ni matangazo.

Matangazo haya huwa yanaoneka kwenye blog yako na utalipwa kadri watu watavyoingia na kuyaona.

(baada ya kutengeneza blog yako utaiunganisha na google adsense ambao wataonesha matangazo kwenye blog yako na kukulipa wewe kupitia bank/cheki au western union)

Njia zingine ni matangazo utakayopewa wewe mwenyewe na makampuni na wafanya biashara ili uwatangazie biashara zao kwa watembeleaji wako

Njia nyingine ni watu kukulipa hili uwawekee post zao mfano blog za mziki wasanii wanalipa pesa ili ngoma zao ziuplodiwe na zisambazwe ivyo ukimiliki blog ya mziki hii pia ni njia muhimu itakayo kulipa

Tazama mfululizo wa video za mafunzo  hapo chini


Somo litaendelea tazama video 👇👇
https://youtu.be/wk1yw3O4CH8

https://youtu.be/ydSoLdNoZFk
https://youtu.be/HL_GVFSyL3A

Jiunge na group lete la whatsapp kujifunza mengi
https://chat.whatsapp.com/JmLFhsS3XOhA7YkAVgvNbH
Share:

Search This site

Follow by Email